Monday, January 14, 2013

tume ya haki za binadamu utetezi wa wanyonge uko wapi- acheni porojo






Hii si haki, utetezi wa wanyonge uko wapi, miaka 50 ya uhuru, na bado porojo nyingi tuu


TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imezitaka taasisi zinazosimamia sheria nchini kuhakikisha zinazingatia haki za binadamu na misingi ya utawala bora ili haki iweze kupatikana  kwa wakati na kwa watu wote.
 
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana, na Kamishina wa Tume hiyo, Bernadeta Gambishi, wakati alipokuwa  akizindua mradi vitabu (Vitini),vya  maboresho ya sheria.
 
Alisema kwa kuzingatia hayo kunaweza kuharakisha  upatikanaji wa haki katika makundi yote ya kijamii nchini, kusimamia maadili na uweled wa maofisa wa sheria, pia ukuzaji wa uhuru wa mahakama.
 
Gambishi alisema kimsingi mradi huo una malengo makuu sita ambayo yatatekelezwa kwa kupitia mkakati wa Kati.
 
 
Akiyataja baadhi maeneo hayo, kuwa ni pamoja na Mfumo bora wa sheria kitaifa: lengo hilo linasimamiwa na Tume ya kurekebisha sheria nchini kwa kushirikiana na taasisi nyingine washirika.
 
Haki za  Binadamu na usimamizi wa haki hili linasimamiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na upatikanaji wa haki kwa walio na uwezo mdogohilo linasimamiwa na Taasisi zisizo za Kiserikali (NGO’S), mfano mmoja ni Chama cha Wana Sheria Nchini (TLS).
 
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Sheria, Reginald Makoko, alisema bado Watanzania wengi wanakabiliwa na uwelewa mdogo wa sheria hali inayowafanya baadhi yao kupoteza haki zao.
 
Hata hivyo, tatizo hilo kwa sasa limepungua kutokana kuwepo kwa vyama vyama vya kisheria ambavyo vinatoa msada wa kisheria bure , malalamiko mengi kuwasilishwa huko.

No comments:

Post a Comment