Na Joachim Mushi
Rukwa
Rukwa
UJENZI wa Shule za Sekondari kwa kila Kata maarufu
kama ‘sekondari za kata’ katika mikoa anuai umeongeza vituko kwenye
sekta ya elimu kwa baadhi ya maeneo kwani kutokana na upungufu mkubwa wa
walimu hasa wa masomo ya sayansi na lugha baadhi ya shule zimefuta
masomo hayo kinyume na taratibu za mitaala.
Miongoni mwa mikoa iliyokubwa na kadhia hiyo ni Rukwa, Wilaya ya
Nkansi ambako baadhi ya shule hizo zimekata tamaa baada ya kukosa walimu
wa sayansi na kulazimika kufuta masomo ya sayansi na kubaki na yale ya
sanaa, licha ya kwamba nayo si yote yenye walimu kwenye shule hizo.
No comments:
Post a Comment