Poleni wanafunzi na jumuiya ya Chuo Kikuu cha DSM (UDSM), ni aibu kwamba
mpaka mgomo na mabomu ndio serikali ichukue hatua kwa madai ya mikopo
kucheleweshwa na kupewa kwa masharti yenye kuumiza watoto wa watanzania
wa kawaida.Kila binadamu anayo haki ya kusoma!Ni moja ya haki ya msingi
ktk haki za kibinadamu. Nasikitika siko pamoja nanyi jimboni Ubungo ktk
wakati huu mgumu, nitachukua hatua za kibunge huku Dodoma-Bungeni.Kwa
Pamoja Tunaweza!!
Shukrani Chanzo za Picha: Mtandao wa JamiiForums
Nimehuzunika sana baada ya kuona picha hizi na habari katika vyombo mbalimbali vya habari. Nipo pamoja nanyi!
Nimehuzunika sana baada ya kuona picha hizi na habari katika vyombo mbalimbali vya habari. Nipo pamoja nanyi!
Maoni Yetu
Rais kikwete, umeleta askari wako watupige chuoni, miliwapiga wazee wa A
mashariki mkawadhalilisha, mmewapiga wamachinga wasio na kipato
wakitafuta walau watakulaje, kama hiyo haitoshi mmetupiga wasomi
tusiseme madai yetu ya msingi. Laana hii itawafata nyuma siku zote na
mwisho wenu hauko utafika. Mmeamua kuila nchi, kuwakandamiza masikini na
kuwarudisha wakoloni kwa kivuli cha uwekezaji, leo rasilimali za nchi
yetu na kodi za wazazi wetu mnagawana na familia zenu na kupanga nani
apate kiasi gani na sisi masikini eti hamna hata hela za KUTUKOPESHA ili
tusome. Kama kweli uko serious na taifa letu, tafadhali tupe mikopo
watoto wa wakulima tusome. TENA JUA KUWA, TANZANIA SIO NCHI YA AMANI,
UNADHANI KAMA WATU HAWAPATI HAKI ZAO, WANA NJAA, WANAKOSA ELIMU NIYO
AMANI? Kama CCM ndivyo ina define amani basi imepitwa na wakati.
Msijifariji kusema tanzania ina amani, yatawatokea puani, si mnafanya
makusudi, kwa kuwa nyie na watoto wenu mna maisha ya kifahari ya pesa za
kodi zetu! Poa yote 9.
MUKANDARA kaonyesha ana uwezo mdogo sana wa uongozi katika kipindi chake cha uongozi. kipindi cha Ruhanga hapakua na huu ujinga, wanafunzi kupigwa mabomu ....... yeye kama Professor anashindwa align na wanafunzi na kuweza kuyatatua haya mambo, na kama ni mambo ya bodi kwa nini yeye aingilie kwa kuita polisi, angeacha wanafunzi wagome mpaka Bodi watoe majibu -yeye hayamuhusu!
ReplyDeleteShame on you MUKANDARA
p.d
KUPIGA WATU AU KUTISHIA WATU HAKUTAZUIA WATU KUDAI HAKI ZAO. TANZANIA SIO NCHI HURU TENA MAANA INAONEKANA UONGOZI WETU WA SASA UNATAWALA KIMABAVU. LAKINI I UNDERSTAND NA WATANZANIA WENGI SASA HIVI WANAELEWA KUWA "FREEDOM IS NOT FREE". I AM READY TO DIE TO BE FREE. ANGALIA YALIYOTOKEA TUNISIA, EGYPT, LIBYA NA NCHI NYINGINE MBALIMBALI DUNIANI. WATU WAKITAKA HAKI ZAO MTUTU HAUWEZI UKASHINDA.
ReplyDeletemi sijui nisemeje kuhusu nchi yetu kwani ni sikitiko sana.viongozi wetu wa upinzani tusaidieni na Mungu wa Mbinguni atawalipa na kam sio hapa basi Mbinguni ambako ndiko kuliko na Makao ya Milele.
ReplyDelete