Showing posts with label udom. Show all posts
Showing posts with label udom. Show all posts

Monday, January 14, 2013

Mikopo ya chuo kikuu -Mitaa Yetu |









Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma - UDOM wamegoma kuingia madarasani wakipinga kile walichodai kuwa ni hatua ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini kuchelewesha mikopo wanayostahili kupata.

Polisi mkoani Dodoma wamelazimika kutumia nguvu za ziada kuwatawanya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma,UDOM waliokuwa wanaandamana kwenda ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma kuwasilisha madai yao.

Dokta Nsekela amewataka wanafunzi hao kuwasilisha hati za madai yao katika ofisi yake na kuahidi kulitatua tatizo hilo ndani ya muda wa siku saba.

lakini baada ya siku saba, tatizo halikututuliwa, na baadaye wanafuzi 900 walifukuzwa na wengine kushatikwa -

chuo kikuu cha dodoma-university of dodoma-Delta Star






Baadhi ya Wahitimu wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa katika harakati za kutafuta picha za ukumbusho na rafiki zao wakati wa sherehe za mahafali ya tatu ya Chuo Kikuu Cha Dodoma yanayotajiwa kuanza saa saba Mchana wa leo katika viwanja vya Chimwaga Vilivyopo Chuoni Hapo